Cookie Consent by FreePrivacyPolicy.com

Refugee Employability Programme

Employability Skills and Integration for Refugees

Refugee Employability Programme

     
  دری  فارسی پښتو English Swahili اَلْعَرَبِيَّةُ ትግርኛ

Boresha ustadi na uwezo wako wa kuayiriwa Kazi

Mpango wa Kuayiriwa kwa Wakimbizi (REP) unalenga kusaidia wakimbizi katika kupata ayira, au ayira bora, katika eneo la Midlands Mashariki. Mpango huu wa usaidizi haulipishwi na unalenga kupunguza vizuizi vya ayira na kuboresha utangamano katika jamii. Limefunguliwa kwa watu wanaostahiki wanaoishi kote Midlands Mashariki, ambayo ni pamoja na Derbyshire, Leicestershire, Lincolnshire, Northamptonshire na Nottinghamshire.

Tunachokupa

Usaidizi wa kuayiriwa uliolengwa na unaoweza kunyumbulika ili kusaidia katika nyanja zote za kuzoea utamaduni wa Uingereza na kupata ayira. Tunatambua kila mchu ni tofauti na tunatoa usaidizi wa binafsi ili kuangazia hili.

Msaada unaweza kuyumuisha:

  • Mafunzo ya lugha ya Kiingereza
  • Ujuzi wa kuayiriwa (Kuandika wasifu, mazoezi ya usaili, mafunzo ya maombi ya kazi)
  • Mwelekeo wa kitamaduni na kusaidia kukabiliana na mahali pa kazi ya Uingereza
  • Usaidizi wa mafunzo ya uyuzi, sifa na kufikia sifa zinazotambulika kwa uyuzi uliopo
  • Usaidizi wa mtandao na kusaidia kutafuta majukumu ya kazi

Vipindi vya usaidizi huwasilishwa kwa njia tofauti na kwa kawaida vitafanyika ana kwa ana katika vituo kote eneo. Katika baadhi ya matukio, vipindi vya usaidizi vinaweza kuwasilishwa mtandaoni. Saa kwa wiki na sifa zitatofautiana kulingana na hali.

Kustahiki

  • Umri wa miaka 18 na zaidi
  • Haki ya kuishi na kufanya kazi nchini Uingereza kama mkimbizi anayetambulika kisheria
  • usiwe katika ayira ya wakati wote (saa 16 awo zaidi kwa wiki) au elimu
  • Kuishi katika Midlands Mashariki

Jua zaidi na uende kuelekea ayira leo!